Utafiti waelezea sababu za saratani
Kifaa cha kubaini saratani
Utafiti mpya unasema aina nyingi za ugonjwa wa saratani ni matokeo ya bahati mbaya, kuliko malezo ya vinasaba, mazingira na mtindo wa maisha.
Watafiti nchini Marekani walichunguza aina 31 za saratani na kugundua kwamba theluthi mbili zilisababishwa na mgawanyiko holela wa seli. Kwa mgawanyiko wa kila seli kuna hatari ya mabadiliko yanayoweza kusababisha saratani.
Wanasayansi hao wanasema kuimarisha mtindo wa maisha na mazingira kunasaidia kudhibiti magonjwa kama ya saratani ya ngozi na saratani ya mapafu.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment